Wanajanvi habari zenu, nina ndugu yangu anataka kuanzisha kilimo cha kisasa cha mboga mboga na matunda hasa mapapai, ameshaanza kuchimba kisima kirefu kwa ajili ya umwagiliaji, swali langu ni kuomba kama kuna mwana janvi yeyote ambaye anafahamu soko katika nchi ya comoro likoje kwa uzoefu, kwani yeye anategemea kuzalisha mwaka mzima kutokana na umwagiliaji, naomba msaada wenu.
↧